FAHAMU UWEZO WA DAMU YA YESU KRISTO
Siku moja usiku nikiwa katika chumba cha hoteli moja hapa hapa nchini,
baada ya kutoka kwenye semina ya kiroho; Roho Mtakatifu alisema ndani ya
roho yangu kuwa; “Fundisha juu ya Damu ya Yesu Kristo”.
Tangu
wakati huo nimekuwa na maombi ya mara kwa mara, nikiomba Roho Mtakatifu
anifundishe juu ya Damu ya Yesu Kristo. Nimekuwa nikisoma na kutafakari
neno la Mungu linalofundisha juu ya damu ya Yesu Kristo. Ni muda umepita
sasa tangu nipate agizo hili. Ndani ya moyo wangu naona ya kuwa muda
umefika wa mimi kuanza kuwashirikisha wenzangu yale ambayo tayari yamo
ndani yangu ingawa ni machache, juu ya Damu ya Yesu Kristo.
Katika mfulilizo wa somo hili,tutashirikiana juu ya mambo manne
tunayopata katika Damu ya Yesu Kristo. Ukweli ni kwamba katika damu ya
Yesu Kristo kunapatikana zaidi ya mambo manne nitakayokushirikisha humu;
lakini kwa sasa naona nianze na haya manne:-
1. Uwezo wa Damu ya
Yesu Kristo katika kuondoa dhambi. Imeandikwa katika kitabu cha 1Yohana
1:9 kuwa; “Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata
ATUONDOLEE dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote”.
2.
Uwezo wa Damu ya Yesu Kristo katika kupatanisha. Imeandikwa katika
kitabu cha Waefeso 2:13-16 kuwa; “Lakini sasa, katika Kristo Yesu, ninyi
mliokuwa mbali hapo kwanza mmekuwa karibu kwa damu yake Kristo. Kwa
maana yeye ndiye amanin yetu, aliyetufanya sisi sote tuliokuwa wawili
kuwa mmoja; akakibomoa kiambaza cha kati kilichotutenga. Naye akiisha
kuuondoa ule uadui kwa mwili wake; ndiyo sheria ya amri zilizo katika
maagizo; ili afanye hao wawili kuwa mtu mpya mmoja ndani ya nafsi yake;
akafanya amani. AKAWAPATANISHA wote wawili na Mungu katika mwili mmoja,
kwa njia ya msalaba, akiisha kuufisha ule uadui kwa huo msalaba”
3. Uzima wa Milele katika Damu ya Yesu Kristo. Imeandikwa katika kitabu
cha Yohana 6:53-54 kuwa; “Basi Yesu akawaambia Amini, amini,
nawaambieni, msipoula mwili wake mwana wa Adamu nakuinywa damu yake,
hamna uzima ndani yenu. Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao
UZIMA WA MILELE…..”
4. Uwezo wa Damu ya Yesu Kristo katika
kutulinda. Imeandikwa katika kitabu cha ufunuo wa Yohana 12:11a kuwa;
“Nao wakamshinda (shetani) kwa damu ya mwana-Kondoo….”
Mtihani
mkubwa sana kwetu sisi wakristo ni kuyaweka katika matendo yale
tunayofahamu katika Biblia. Nakushauri kwa Jina la Yesu Kristo kuwa uwe
mtendaji wa neno, na usiwe msomaji tu.
Ni maombi yangu kwa Bwana ya kuwa Roho wa ufahamu wa Bwana atakuwa juu yako. barikiwa sana BY MWL CHRISTOPHER MWAKASEGE
Post a Comment