0
     MKE MWEMA NI WANAMNA GANI?
     
      



  Vijana wengi wamekuwa wakijiuliza mke mwema au mme mwema ni wa namna gani na anasifa zipi. Hayo yamekuwa ni maswali yao kila kukicha na wengine wamefika hatua ya kuogopa kuanzisha mahusiano au kuingia katika mahusiano kwa sababu ya changamoto mbalimbali ambazo wamekuwa wakiziona kwa wale walio katika mahusiano ,hilo limekuwa shida kwao. Napenda kukufundisha mbinu za kuweza kukusaidia kumtambua mwenzi wako wa maisha na nilipi la kufanya pale unapoziona sifa zile unazozitaka.


                  SIFA ZA MKE NA MME MWEMA

Kila mtu amekuwa na sifa zake mwenyewe lakini tunaweza kuangalia zile za mhimu ambazo unatakiwa kuzitambua.

 1. Mke au Mme unaye mtaka anapaswa awe mcha Mungu.

hii ndiyo sifa kuu na yakuzingatia,kijana kabla ya kuoa au kuolewa ni vizuri atambue kuwa mme au mke atakaye weza kubeba ndoto zake ni yule ambaye anamcha Mungu yani mwenye hofu ya Mungu. kijana wa kiume au wa kike mwenye sifa hii ni mzuri sana tena sana kwa sababu zifuatazo:

     a). mke/mme mwenye hofu ya Mungu hawezi kutoka nje ya ndoa na hawezi kuwa mwenye hasira ya kulipiza na hawezi kukuwazia mabaya hata ukikosana naye atakuwa mwepesi kukusamehe na kusahau.

    b). Hawezi kuwa mwongo, hii ni changamoto ambayo huweza kujitokeza mara kwa mara kati ya wana ndoa lakini kama wakiwa wacha Mungu wataogopa kusema uongo au kujenga mahusiano katika msingi wa uongo. Napenda kushauri wale wanaotegemea kuwa katika mahusiano au waliokwisha ingia waepuke kusema uongo kwani madhara ya uongo ni kupotea kwa uaminifu ndani ya moyo wa yule unayeishi naye au unayetegemea kuishi naye,jarbu kufikiri mke au mme anakuambia anasafiri kwenda kwa shangazi yake lakini unaambiwa hakwenda kwa shangazi alienda kwa rafiki yake utaweza kumwamini? jibu ni hapana lazima moyo utajeruhiwa nakuonya kijana unayetaka kuwa katika mahusiano kwepa kujenga mahusiano katika uongo kwani madhara yake hayafutiki.

    c). Mcha Mungu anakuwa mtii.

Hakuna kitu kizuri wanaume wanapenda kama kupata mke aliye mtii, utii wa mwanamke hupunguza ugomvi na hasira pale panapotokea sitofahamu. Mabinti wengi wamepoteza wachumba wao kwa kukosa utii,ndoa nyingi zina migogoro isiyoisha kwa sababu hakuna roho ya utii miongoni mwa wana ndoa.

    d). Mcha  Mungu haogopi na haoni aibu ya kuomba msamaha.

Neno nisamehe ni nino dogo lakini likikosekana kwa wanandoa ndoa hiyo inakuwa moto, vijana jifunze kuomba msamaha pale unapokuwa umeona kuna mitafaruku imetokea kati yenu.

    


   Ndugu msomaji wangu kuatilia mwendelezo wa somo hili wiki ijayo. Ukiwa na maswali au unahitaji maombi na ushauri wasiliana nami kwa namba 0759762229

       Somo limeandaliwa na :

       Mwl. elisante daudi

Post a Comment

 
Top