0
     Kila mtu anapenda kufanikiwa katika maeneo tofauti tofauti ambayo anatamani afanikiwe. Mtu anaweza kutaka afanikiwe katika mambo mbalimbali inaweza kuwa katika Elimu,Biashara,Huduma ya uimbaji, Kuwa mhubiri wa kiwango fulani.Yote hayo hutokana na yale mtu anayowaza na kutamani ambayo wakati mwingine huitwa maono au ndoto. Utasikiwa kila mtu akisema ana ndoto au maono akiwa na mana ya mafanikio ya kuwa na kitu furani katika maisha yake
   Nivizuri na inapendeza kila mtu Kuwaza namna atakavyoweza kufanikiwa katika yale anayotaka na kukusudia  awe nayo.
              MAMBO 6 YA KUKUSAIDIA UFANIKIWE
    1. Penda kuwa nalo hilo unalotaka uwe nalo.
Hauwezi kuwa na kitu usichokipenda, ili uwe na nyumba sharti upende kuwa na nyumba,ili uwe na elimu sharti upende kwenda shule kusoma,ili uwe na biashara sharti upende kuwa na biashara. Kila kitu utakipata pale unapofungua moyo wako kukipenda au kukitaka kitu hicho.
  2. Tafuta elimu juu ya neno hilo unalotaka kufanikiwa
hii ni hatua muhimu sana kwako kwa sababu lazima uwe na ufahamu juu ya hilo jambo unalotaka, linapatikana vipi,je,kuna watu walionalo hilo? je,wenzako wamefanikiwa kwa kiwango gani juu ya hilo? Hayo ni maswali ya muhimu sana
 3. Hesabu gharama ya namna ya kulifanikisha hilo
Hauwezi kukurupuka kujenga nyumba au kufanya biashara kama haujajua kiwango cha fedha utakachotumia kufanikisha hilo au kiyo ndoto yako.
 4.Tafuta marafiki waliokwisha fanikiwa juu ya hilo.
Kwa kupitia hao unaweza pata uzoefu na mbinu walizotumia kufanikiwa,pia unaweza kujifunza maeneo yaliyowahi kuwatatiza wasifanikiwe haraka,
 5. Usiogope changamoto na upinzani.
Mara nyingi tambua hili kila unalowaza si watu wote wanaweza kukufariji na kukuhamasisha nakukufariji wapo watakao kukatisha tamaa na pia changamoto nyingine inaweza kuwa mazingira au ugumu wa kazi,azimia kutokukata tamaa
 6. Jiamini kuwa unaweza kulifikia lengo lako. 
Katika kujiamini ndipo kunamafanikio.

      SOMO: limeandaliwa na
       Mwl   :Elisante Daudi
     CONTACT: +255759762229

Post a Comment

 
Top