FURAHIA MAISHA YA IMANI
Kwa mjibu wa maandiko imani chanzo chake ni kusikia na kusikia huja kwa neno la Mungu.
Waebrania 11:1 inasema "Basi imeni ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo na nibayana ya mambo yasiyo onekana" Ndugu yangu kwa andiko hilo unaweza kuona na kujifunza mambo ya msingi tena siri kubwa sana nayo ni haya yafuatayo:
1. kuwa na uhakika. hii ni hatua ya msingi sana lazima ujue kuwa kile unachokifikiria kipo na kunawatu ambao wamewahi kufanikiwa kuwa nacho, ukishajenga uhakika huo ndipo wazo lako la kukusudia kuwa na hicho kitu litakuwa imara na utaanza kuchukua hatua za msingi kulipokea neno hilo. Hii ni mhimu uelewe mtu wa Mungu ukijua siri hii utakuwa umefanikiwa. lazima ujue hayo.
2. Ni miongoni au bayana ya vitu visivyo onekana .
Imani huwa ni wazo linalokuwa ndani yako mfano unawaza kujenga nyumba, kufungua biashara,kuwa na usafiri lakini wakati huo hauna mtaji wa kuwa na kitu hicho lakini kwa kuwa hatua ya kwanza uliweka msingi wa kuamini kwamba hilo uwazalo lipo basi utashangaa nafsi yako inajenga tabia ya kutafuta watu waloifanikuwa kuilpata hilo unalotamani uwe nalo,na utajalibu kfikiri hatua za kuchukua kwa lengo la kufanikiwa kufikia leongo lako. Wakati huo utapaswa kujenga wazo lazima ufanikiwe lazima ufanikiwa kwa hiyo hatua Mungu anacho fanya nikukuongoza na kuitunza afya yako ufikie lengo lako hilo,Mungu ataachia ufunuo halisi namanisha wazo halisi la kuweza kufanikisha wazo lako hilo.
3. Matarajio.
Jambo la tatu katika andiko hilo ni matarajio yani matokeo ya kile ulicho kiamini na kukisimamia. hii ndiyo hatua ya mwisho au timizo la kusudi la moyo wako, watu wengi huwa wanapenda kuona matokeo ya kile walicho kiamini. Ahimidiwe Mungu aliyetoa tangazo hili kuu kwamba ukiamini yote yanawezekana, ukiamini kwa msingi wa andiko hilo utapata yle unayotaka.
Nakumbuka miaka ya nyuma najifunza somo hili, niliwaza na kuamua kujenga wazo la kuamini, nilijenga wazo la kumiliki kiwanja katika maeneo ya wilaya yangu kiwanja kizuri nikafanya maombi na kuomba Mungu anipe kiwanja, wakati naomba niliwaza kuamini kuwa Mungu amenipa tayari kiwanja hicho, sikuishia hapo kuamini kuwa maombi yamgu yamejibiwa sawa na maandiko yanavyosema niliamua kuchukua hatua ya kuulizia wapi viwanja vinapatikana na wakati huo sina fedha na sijui fedha nitapata wapi nakumbuka sikukata tamaa bali niliendelea mbele na msimamo wangu wa kutafuta kiwanja, nikaambiwa kuna mtu anacho na kilikuwa kizuri wazo likaja sasa Mungu kiwanja nimepata ndiyo napata wapi fedha,sikukata tamaa nipatana bei na mwenyekiwanja nikiwa njiani natoka kwa mwenye kiwanja nlikutana na mzee mmoja mfanya biashara aliyekuwa ananifahamu akaniuliza mbona unaonekana una mawazo? nikamjibu kunakiwanja jizuri nimepata lakini fedha sina akaniuliza bei nikamwambia akaniambia nitakupatia hiyo fedha ukichukue Haleluya ndipo nilijua MUNGU ana namna tofauti tofauti ya kukupatia yale uliyo yaamini.
MAMBO YA KUZINGATIA
a . Tambua neno hili kila unaye mwona amefanikiwa au ungetamani kufikia hatua ya maisha aliyo nayo jua kuwa alizaliwa hana kitu hicho kama unavyomwana isipokuwa aliamua kuamini kile alichonacho kuwa kunasiku atakuwa nacho. Chukua hatua ya kuamini.
b.Tafuta urafiki na wale waliofanikiwa katika lile jambo unalotaka Mungu akupatie,
c. Jenga tabia ya kununua vitabu au kusoma blog zenye mafundisho juu ya kufanikiwa kupata hicho unachokitaka
d. Endelea kumwomba Mungu na kusoma maandiko yanayoeleza jambo hilo ni lako.
SOMO limeandaliwa na:
REV. ELISANTE DAUDI
Contact . +255759762229
Post a Comment