0

FUMBUA MACHO UONE MBINU ZA KUPATA FEDHA KWA KUUZA MAUA

Kumekuwa na manunguniko kati ya watu wengi wakiwaza watatumia njia gani kutengeneza fedha, napenda kukupa elimu na mbinu za kujipatia na kujiongezea kipato kwa njia ya uuzaji wa maua.

                      Hakuna mtu asiyependa maua, maua hutumika kama kivutio kikubwa cha maeneo mbalimbali ,kila nyumba utakayo itembelea utakuta maua ndani ya nyumba au nje ya nyumba,kila sherehe au kumbi za mikutano utakuta maua hii ni ishara tosha kuwa maua ni mhimu na yanahitajika.
Hakuna nchi isiyo hitaji maua tena kumekuwa na wafanya biashara ambao wamekuwa wakisambaza bidhaa zao nje,mataifa makubwa na madogo duniani yanahitaji kuona maua . 
Napenda kukuhamasisha uone umhimu wa biashara hii kwani haitaji mtaji mkubwa ni mtaji wa kawaida ila muda na nguvu kwanini nakuambia haihitaji mtaji mkubwa?
Nimekuambia haitaji mtaji mkubwa kwa sababu ifutayo:
Zipo mbengu za maua ambazo hupatikana kwa uurahisi kazi yako inakuwa kupandikiza au kuotesha .
Faida za uuzaji maua     
Zipo faida mbali mbali unazoweza nufaika nazo kwa biashara hiyo mfano unaweza kuzarisha miche elfu moja na kila mche unaweza kuuza kwa bei tofauti kulingana na hadhi ya ua lenyewe, jaribu uchukulie bei ya sh,500 kwa mche na uzalishe miche 1000 utapata kiasi cha sh,500000/= kumbuka hiyo ni bei ya makadirio ya chini waza kwa yale maua yanayouzwa mche 1500 na kuendelea.
Nalotaka kukuhamasisha zingatia yafuatayo muda wakupandikiza miche hauzidi mwezi hadi miezi miwili lakini zikisha ota tayari unauhakika wa kuvuna fedha.
 Huenda wewe ni mfanya biashara ya maua na unapenda nikutafutie soko la maua yako usisite kuwasiliana nami kwa namba zinazopatikana kwenye blog hii, aidha unaswali unapenda kuuliza au msaada wa ushauri usisite kututafuta.
       Imeandaliwa na ;
            Mwl. Elisante Daudi
       contact: 0759762229









Post a Comment

 
Top