MHE.RAISI MFANO MZURI WA KUIGWA
Mhe. Raisi JOHN POMBE MAGUFURI
Tanzania inajivunia kuwa na kiongozi mwenye kujari na kuhimiza maendeleo ya wananchi wake. Napenda kumpongeza Mheshimiwa Raisi wetu kwa kazi kubwa anayoifanya. Kupitia maisha yake ninayomengi ninayoweza kujifunza na hata wewe msomaji wangu Nihaya yafuatayo.
1. Usimdharau mtu au binadamu mwenzako wakati haujui atakuwa nani siku za mbeleni.
Umesha jiuliza watu waliokuwa wakisoma naye enzi za utoto, huenda walikuwa wakimwona wa kawaida tu laiti wangejua atakuwa nani yamkini wangejari mahitaji yake na kufuatilia maendeleo yake kwa karibu sana.
Tazama picha ya mheshimiwa enzi za ujana
2. Pamoja nakuwa hakuna mtu aliyejua atakuwa nani badaye bado yeye hakujidharau kwa kuwa hakuna anajua atakuwa nani bali alijenga hali ya kujiamini na kuthubutu kujaribu kupigania ndoto zake. kwa hilo napenda kukushawishi msomaji wangu usikate tamaa kwa kuwa hakuna anaye kujua wewe ni nani bali angalia ndoto zako kwa kujifunza kwa Raisi wetu mtukufu.
3. Msimamokatika yale unayo yaamini.
Kati ya vitu ambavyo najifunza kwa Mheshimia ni Msimamo katika yale anayoamini.. Kwa hilo nimependa sana kwani kiongozi hawezi kuwavusha watu anaowaongoza kama hatakuwa na msimamo katika yale anayo yaamini, je,unataka uwe kiongozi bora? Jenga tabia ya kusimamia kile unachokiamini madamu ni kwa ajiri ya manufaa kwa wengi.
4. Hakubagua kazi. Kiongozi mzuri ni yule ambaye habagui kazi bari atajishughulisha na kazi yoyote madamu inaleta faida mfano, amekuwa mwalimu kwa miaka kadhaa hii inaonesha hakuchagua kazi. Kama unataka kufanikiwa usiwaze kuanza na mambo makubwa anza na madogo ili uweze kupata makubwa.
Kwa hayo machache unaweza kuwa umepata ya kujifunza. Tunazidi kumuunga mkono Mheshimiwa kwa kipindi chote cha uongozi wake na tupo tayari kusimamia kauli mbiu ya HAPA KAZI TUUU
Imeandaliwa na :
Mwl. Elisante Daudi
Contact : 0759762229
Post a Comment