0

Mambo unayostahili kufahamu kabla ya kuanza biashara Yako

Nimatumaini yangu kuwa ungependa kujikwamua kiuchumi na kufanikisha ndoto yako, watu wengi utawasikia wakilalamika serikali haiwajari naposikia manunguniko hayo huwa najiuliza kwanini unapenda kubebwa na wakati kuna njia rahisi ya kufika katika ndoto zako. wasomi wengi hawana kazi za kufanya  kwa sababu wanapenda kuwaza mambo makubwa mfano kumiliki kampuni lakini  wanasahau kuwa hauwezi kufikia lengo kubwa kama hauna uzoefu na mambo madogo. Leo chukua hatua kwa kuzingatia haya yafuatayo:
  1. Waza kuuza  kile wateja wako wanataka: 
    Usijaribu kufikiri kuagiza yani siangazie tu kile unachotaka. Usipotafakari kuhusu wateja wako,kuna uweza wa kutonunua bidhaa yako. Hakikisha unatafiti soko ili kujua kama huduma au bidhaa yako ni ya maana na nafuu kwa uwezo wa wateja.
  2. Uujue uwezo wako: 
    Angazia sana sana yale unayoyafanya vizuri na uwache mengine. Hustahili kujua majibu yote wala kukusanya maswala yote .Kuwa mwaminifu kwa yale unayoweza kutekeleza na yale usiyomudu kutekeleza. Kumbuka, ni vizuri kuomba msaada iwapo hujui kitu Fulani.
  3. Fanya utafiti wako: 
    Tumia madarasa, hafla au semina, vitabu na kanda ili kujifunza yale unayoweza kabla hujaanza biashara.Kama hujui chochote kuhusu uendeshaji wa biashiara, kuna mafunzo mengine ya malipo ya chini, vitabu na kanda.Jaribu maktaba ya mahali pale unapoishi ama hifadhi ya vitabu, na uulize yale yote usiyoyafahamu kuhusu soko, nguvu na uwezo wako, mahali halisi na yale watu wanataka.
  4. Tegemea juhudi zako: 
    Unahitaji kuwa macho katika bajeti yako, la sivyo, utaishia katika madeni makubwa ama utoweke kutoka biasharani haraka sana. Kama huwezi kupata kila kitu unachokiitaji sasa hivi, wachana nacho na ufikirie zaidi kuhusu mpango wako.
  5. Unda mpango wa mauzo: 
    Hili ndilo swala nyeti la kuwavutia wateja wako. Toa ramani ya jinsi ya kupata wateja wa kutumia bidhaa au huduma yako na namna utakavyowasawishi warejee. Unastahili kujiuza ili watu wakujie.
  6. Huwezi kushughulikia biashara peke yako: 
    Unapokuwa na watu wengi wa kukusaidia na vitu “vidogovidogo”,ndivyo utakavyochukua muda mwingi kunawiri biashara yako. Usiogope kuomba usaidizi na ushauri kutoka kwa rafiki zako na hata watu wa familia

Post a Comment

 
Top