HISTORIA YA HUDUMA YA ASKOFU ZACHARIA KAKOBE (1)
BWANA
YESU asifiwe Mwana Maisha ya ushindi mwenzangu. Kuanzia leo nakuletea
Historia ya kuvutia sana ya huduma ya Askofu Mkuu wa FGBF Zacharia
Kakobe, Nimependa sana kukushirikisha na wewe maana kihuduma kanisa hilo
mwaka huu wameadhimisha miaka 25 ya huduma tangu lianzishwe Mwaka 1989,
usikose hapa hapa hapa Maisha ya ushindi blog.
Karibu sana
Askofu Zacharia Kakobe ni mwanauamusho
wa kimataifa, na mwanzilishi wa Bishop
Zachary Kakobe International Ministries (BZKIM), shirika lisilo la
kibiashara la kiimani , lililosajiliwa Marekani. Pia ni mwanzilishi na Msimazi
Mkuu waFull
Gospel Bible Fellowship Church,
lenye usajiri wake nchiniTanzania. Anachunga kanisa lenye maelfu ya waumini
jijini Dar-Es-Salaam, Tanzania; ambalo ni kanisa mama; ambalo kwalo, anasimamia
zaidi ya matawi 400 (matawi), ambayo aliyaanzisha kwa kuyatawanya katika mikoa
na wilaya zote za Tanzania bara.
Askofu
Zakaria Kakobe ni Mtanzania; alizaliwa siku ya Jumatatu, Juni 6, 1955; huko Kibondo,
Tanzania. Safari yake ya kiroho ilianza Jumapili ya Pasaka, Aprili 6, 1980;
siku alipozaliwa kiroho wakati mkutano wa Miujiza ya Uponyaji kanisani, vilivyoendeshwa
nchini Tanzania na Mwinjiristi mashuhuri wa Kitaifa Askofu Moses Kulola, katika kanisa laTanzania Assemblies of God, Ilala,
Dar-Es-Salaam, lililokuwa likichungwa na Mchungaji Titus Mukama. Jioni ile, ujumbe
wa kiinjili ulioukuwa ukihubiriwa na Askofu Moses Kulola, ulimfanya Zakaria
Kakobe kwenda madhabahuni kuombewa , kwa ajili ya Kuokoka. Alikwenda mbele ya
kanisa akilia kwa uchungu waziwazi, na kutubu dhambi zake; akiwa na kusudio halisi
toka ndani ya moyo wake , kuacha dhambi, na anasa; na kumpokeaYesu ndani ya
moyo wake kuwa Mtawala Mkuu na Mwokozi wake.
Tangu
siku hiyo, maisha yake yalibadilika kabisa.Mkewe na marafiki zake waliomfahamu
kabla, walishuhudia na kuthibitisha kwamba maisha yake yalikuwa yamebadilika.
Alikuwa amezaliwa tena.Alikuwa ni mtu mpya, katika Kristo. Mda mfupi baadae
alijiunga na kanisa la Tanzania
Assemblies of God, Temeke, Dar-Es-Salaam; kanisa alilokuwa akisali Kwa
miaka kadhaa, alikuwa ni mshirika mwaminifu wa kanisa hilo, na mchungaji wake
alikuwa ni hayati Callist Masalu, ambaye alikuwa ni Mtumishi wa Mungu mashuhuri
nchini Tanzania kwa zaidi ya miongo minne.
Wito
wa uchungaji wa Askofu Zakaria Kakobe ulikuwa ni wa kipekee, au kwa lugha rahisi,
ulitokea kimiujiza. Mnamo mwaka 1982, Yesu Kristo mwenyewe alimtokea kwa
nyakati mbili tofauti sebuleni, kumpa ujumbe Wake wa kumuita kwenye uchungaji. Kwa
nyakati zote Yesu alimtokea sebuleni mapema usiku, mapema kabla ya mda wa
kulala wakati shughuli za kawaida zilikuwa zikiendelea sebuleni. Katika tukio
la kwanza, Yesu alibisha hodi kwenye mlango uliofungwa vizuri, na kabla mda wa
kufungua mlango, alipita kwenye mlango ule bila kuufungua.Alivyoingia , taa za
sebule zilizima, bila kuzimwa na mtu yeyote, na utukufu Wake ukaangaza. Kisha
akakaa na kusema “Msigope, Mimi ni Yesu”. Kisha akasema ya kwamba anamtuma
Kakobe kuhubiri Neno Lake.
Aliendelea
kusema kwamba, Kakobe, atakuwa Mchungaji wa kundi kubwa la kondoo, na
atawatunza na kuwalisha maelfu ya kondoo na wanakondoo; na kwamba atayaangalia
makundi mengine mengi ya kondoo. Wakati huohuo, atahubiri Injili kwa mataifa,
katika mataifa mengi duniani, huku ishara za uweza na maajabu zikimfuata kokote
alikoenda kuhubiri Neno Lake. Aliongea sana kuhusu vitu vingine vihusuvyo
mpango wa Mungu kuhusu maisha na uchungaji wa Kakobe, na Akahitimisha kwa
kumsihi tena na tena, kuwa mwaminifu kwake hadi mwisho; ili avione vitu vyote
hivi vikitimia, ndani ya uchungaji wake. Baada ya hitimisho, hakumpa nafasi ya
kujadiliana. Kisha akaondoka kupitia mlango ule ule, kwa namna ile ile, na papo
hapo, taa za sebule zikawaka tena zenyewe.
Katika
hali ya kushangaza baada ya kupokea ujumbe, Kakobe aliitikia kwa kuukataa wito
wa Yesu Kristo. Katika majadiliano ya hisia na mkewe Hellen, Kakobe alimwambia
mkewe, “Samahani, siwezi kuwa mhubiri wa msalaba wala mchungaji. Sina mpango
kabisa na aina hii ya utumishi. Mpango pekee ni kuja kuwa mfanyabiashara
mkubwa, na kutumia pesa zangu kuendeleza injili ya Yesu Kristo. Si zaidi wala
pungufu ya hapo!”.Kwa wakati huo, Kakobe alikuwa akihusika katika misaada ndani
ya Kanisa, Tanzania Assemblies of God.
Alimsaidia mwinjilisti wa Tanzania, Askofu Moses Kulola, kuanzisha utumishi wa kurekodi
na alikuwa akitumia vifaa vyake vya kielektroniki kurekodi jumbe zake za injili na kusambaza
tepu za mahubiri kwa wasikilizaji wengi; kwa gharama zake mwenyewe. Alikuwa na
jukumu la kusambaza Neno kupitia tepu za mahubiri za Askofu Kulola.
Alikuwa
pia ni mwenzi ndani ya utumishi wa Askofu Kulola. Alitakiwa kujitoa kwa kadri
ya uwezo wake, kwa ajili ya injili ya Ufalme. Hakuwa kabisa na fikra za kuwa
mhubiri wa neno la msalaba katika kanisa lake la Assemblies of God alikokaa, hakuwahi
kupangiwa kuhubiri wala kufundisha. Alikuwa ni muumini wa kawaida tu wa kanisa.
Alimwambia mke wake,“ Kama Yesu akinipa nafasi ya kujibu wito wake, jibu langu
litakuwa, sina nia ya kuja kuwa mchungaji wala mhubiri wa mikutanoni, na
nitamwomba anipe uwezo wa kupata mali; ili niwafadhili vya kutosha Wahubiri wa
Injili.
Miezi
kadhaa baadae, mwaka uleule; Yesu alikuja tena katika makazi ya Kakobe, katika
namna ile ile. Katika ujio Wake wa pili, alichukua mda mfupi kuelezea mpango wa
Mungu kuhusu maisha ya Kakobe na huduma yake; lakini mara hii kwa msisitizo
zaidi; na kisha akahitimisha kwa kusema kwamba itachukua mda mrefu zaidi kwa
Yeye kurudi tena katika namna ile; na baada ya hapo akaondoka.
Ujio
huu wa pili wa Yesu ulileta maendeleo chanya kwa Kakobe kimwitikio wa wito? La
hasha! Kakobe aliendelea na msimamo uleule kwa miaka kadhaa, bila kupunguza.
Hadi ikafika mwaka 1987, mnamo mwezi wa kumi na moja, wakati Mwinjilisti wa
Kimataifa, mwenye upendo na Afrika, Reinhard Bonnke, aliitisha mkutano wa
injili Dar-Es-Salaam, Tanzania. Mkutano huo ulivuta maelfu ya watu kutoka
sehemu zote za nchi. Kakobe alikuwa mmoja wa walioongoza mkutano huo. Siku ya
mwisho ya mkutano, kulikuwa na uamusho mkubwa wa roho wa Mungu. Watu maelfu
walimpokea Yesu , na miujiza mingi ikatokea. Mhubiri alipokuwa akihitimisha,
Kakobe alitumia mda kutafakari makundi ya watu, upokewaji mwingi wa Yesu Kristo,
na miujiza iliyotokea, ambayo ilimtukuza Yesu Kristo jijini na nchi nzima kwa
ujumla. Wakati akitafakari mambo haya, kutokewa mara mbili na Yesu Kristo
kulikomtokea sebuleni kwake, miaka mitano nyuma, kukamrudia tena akilini mwake,
na ghafla akasikia sauti ndogo tulivu ikisema moyoni mwake na kusema,
“Mwanangu, mhubiri sasa yu auaga mkutano, ambao utaendelea kulitukuza Jina
Langu, baada ya kuondoka kwake?”Baada ya sauti hii nini kilitokea?Kwa maneno
yake mwenyewe Kakobe anasimulia, “Sauti hii iliupondaponda moyo wangu, na
kutetemesha mifupa yangu yote.Nilikuwa
sijiwezi. Wakati makutano walipoimba nyimbo za furaha za kusifu
kuhitimisha mkutano, sikuweza kuimba nao, badala yake, nililia kwa uchungu kwa
sauti yangu ya juu. Nilitubu utukukutu wangu wakutokutii wito wa Bwana,
nakumshukuru kwa kunivumilia na nikayapokea mapenzi yake, na nikasema, Ni hapa
Bwana, nitumie Upendavyo. Kisha Roho wa Bwana akinijaa kwa uweza mkuu, na
ghafla nijazwa nguvu ya Roho Mtakatifu; ujasiri, imani na utashi wa ndani kwa
ndani wa kuhubiri Neno na kuwaombea wagonjwa na wenye uhitaji. Sikuweza
kusubiri siku nyingine kulihubiri Neno Lake katika Mikutano ya Miujiza ya
Uponya!"
Baada
ya maandalizi muhimu ya kiroho, siku iliwadia.Hiyo ilikuwa Agosti 3, 1988;
wakati Kakobe alipoanza safari yake ya uhubiri. Na timu yake ya wainjilisti,Gospel Evangelistic Team (GET), alienda
mikoani kuanzisha mikutano mfululizo ya miujiza ya uponyaji, kwa mialiko kutoka
makanisa mbalimbali ya Kipentekoste. Alifanya jumla ya mikutano ya wazi kumi
Tanga, Kilimanjoro, Tabora, Mbeya, Pwani na Dar-Es-Salaam; nchini
Tanzania.Akizungumzia mafanikio ya mikutano hii, mchungaji mmoja mkongwe
alisema, "Hii mikutano kumi ya kwanza katika huduma yake imethibitisha
kuitwa kwake." Katika mikutano yote hii, mwitikio ulikuwa juu ya wastani
maradufu.Mamia ya watu walimpokea Yesu Kristo, katika kila mkutano, na miujiza
mingi ilitokea.
Akizungumzia
miujiza ya ajabu, iliyotokea katika mikutano yake kumi ya kwanza ambayo hawezi
kuisahau; Askofu Zakaria Kakobe alisema hivi, “Siwezi kuisahau miujiza miwili
ya ajabu.Wa kwanza ni muujiza wa ajabu ambao Bwana alifanya katika mkutano
niliofanya katika viwanja vya soko la kijiji cha Hedaru, mkoani Kilimanjaro;
kuanzia Jumamosi, Agosti 13 hadi Jumatatu, Agosti 15, 1988. Mkutano huu ulikuwa
umefadhiliwa Swedish Free Mission Church.Katika
siku ya kwanza ya mkutano, wanakijiji walikuwa wagumu kuja karibu na viwanja
vya mkutano kwa sababu hawakuamini katika miujiza; ndipo ghafla, nikawa
nimejazwa aina flani ya imani isiyo ya kawaida iliyonitaka kuzungumza na watu waliokuwa kwa mbaali, na
kuwaambia kumleta kiwete yeyote aliyefahamika kwa wanakijiji wote, na mara tu
baada ya maombi kiwete huyo atainuka na kutembea.
Soma ushuda wa ndugu anaeleza matendo makuu ya Mungu kupitia huduma hii: palikuwa na mwanamke ambaye alikuwa na umri wa zaidi ya miaka
40, alikuwa ni kiwete toka tumboni mwa mama yake. Wanakijiji wote walimfahamu mama
huyu. Walimpeleka kokote alikotaka kwenda kwa sababu hakuweza kujikokota wala
kutambaa, achilia mbali kusimama mwenyewe na kutembea! Kwa harakaharaka walimleta
karibu yangu, na wakasema, “Mhubiri, kama mama huyu atasimama na kutembea, basi
tutaamini mahubiri yako” Kisha nikasema, “Kitu flani kisicho cha kawaida
kinaenda kutokea, hapahapa, sasa hivi! Nawasubiria tuu watu wote waliosamama
huko mbali.Tafadhali jongeeni karibu, na muone muujiza huu kwa macho yenu
wenyewe.”Punde tuu, baada ya viwanja vya mkutano kufurika mamia ya watu ambao
waliokuwa mamejaa shauku. Ndipo nikasema kwa ujasiri, “Mama huyu anakwenda
kuamka na kutembea sasa hivi.” Baada ya kusema maneno haya uoga uliniingia,
nilitetemeka, na mifupa yangu yote ilikuwa ikitetemeka. Aina hii ya utumishi
ilikuwa ni mpya kabisa kwangu! Nilikuwa najifunza somo la namna ya kutumia
karama za Roho Mtakatifu; katika Shule ya Roho Mtakatifu.Kisha nikasikia sauti
ndani yangu ikisema, “Leo, utaaibishwa kwa sababu umesema kitu ambacho
hakiwezekani. Utumishi wako unakwenda kuchafuliwa mara moja.”
Punde
baadae, nilimuona mmoja wa nilioambatana nao, aliyekuwa akicheza kodiani, kabla
sijachukua amdhabahu kuhubiri; taratibu akiondoka kuificha nafsi yake, Kisha
nikasikia sauti tulivu ndani yangu ikisema, Usiogope, mtumishi wangu, maana
Niko pamoja nawe. Sema neno la maombi tu na Nitafanya yanayobaki” Sauti mpya
ilinifanya niisahau ya mwanzo, lakini nikaamua kufumba macho wakati nikiomba,
ili nisione yaliyokuwa yakiendelea eneo hilo. Ndipo nikasema neno la maombi.
Nilipomaliza kuomba, niliamua kuacha macho yangu yamefumba, ili nisione
yaliyoendelea. Kisha ukafuata ukimya mfu, na kisha baadae, vifijo, na kelele
kuu- aina ya pekee ya juu ya kuimba kwa tetemo inayotumiwa sana na wanawake
Afrika na katika tamaduni nyingine, kama ishara ya furaha-iliyonifanya nifungue
macho! Na unajua nini!Yule mama alisimama kwa miguu yake kwa mara ya kwanza
katika maisha yake na kuanza kutembea. Umati ulikuwa umepamba moto kwa kelele
za shangwe na kelele za haleluya! Taarifa za muujiza zilisamba kwa kasi kwa
kuongea kwa watu kulikofanya watu wajae toka pande zote hata yule mcheza kodiani alitoka mafichoni! Kila mmoja
alitaka kuona muujiza kwa macho yake wenyewe! Yesu alikuwa hai na halisi kwa
kila mwanakijiji, na baada ya hapo wanakijiji waliamini kila neno
lililohubiriwa. Miujiza ya kustajabisha iliendelea kuwa mada ya kijiji kwa
miaka kadhaa baada ya mkutano.Pia, muujiza uliamsha imani yangu na kunifanya
kumhubiri Yesu katika mikutano iliyofuata imani kubwa moyoni mwangu, isiyowahi
kutokea kabla.
Post a Comment