0

Rais Obama atembelea mji wa Hiroshima

  • siku ya leo
 
Image caption Obama akiwa Japan
Rais Barrack Obama amekuwa rais wa kwanza aliye mamlakani nchini Marekani kutembelea mji wa Hiroshima tangu shambulio la nuklia wakati wa vita vya pili vya dunia.
Obama amesema kuwa kumbukumbu za tarehe 6 mwezi Agosti 1945 hazifai kusahaulika,lakini hakuomba msamaha wa shambulio hilo la Marekani ikiwa ni bomu la kwanza la kinyuklia kutumika duniani.
Image copyright Reuters
 
 
Image caption Obama akiwasili mjini Hiroshima
Bw Obama alizungumza na baadhi ya walionusurika na katika hotuba yake akayataka mataifa kujiendeleza bila silaha za kinuklia.
Takriban watu 140,000 walifariki mjini Hiroshima na wengine 74,000 siku mbili baadaye katika bomu la pili katika mji wa Nagasaki.
Image copyright AFP
 
Image caption Obama akiweka shada la maua katika makavazi ya kumbukumbu ya Hiroshima
Bw Obama alitembelea makavazi ya Heroshima kabla ya kuelekea katika eneo la kuhifadhi kumbukumbu za shambulio hilo,akiandamana na waziri mkuu Shinzo Abe.Wote wawili walisimama mbele ya mwanga wa milele.

Post a Comment

 
Top