Nigeria yaanza kuwapatia fedha raia masikini
3 Januari 2017
Serikali ya Nigeria imeanza kusambaza mpango mpya wa kuwapa fedha za kila mwezi, watu milioni moja maskini na wasiojiweza katika jamii.
Serikali ya Nigeria imeanza kusambaza mpango mpya wa kuwapa fedha za kila mwezi, watu milioni moja maskini na wasiojiweza katika jamii.
Hatua ya kwanza ya kutolewa kwa mshahara huo, ambapo kila mtu atapokea dola 16 kwa mwezi, imeanza katika majimbo tisa kati ya majimbo 16 nchini Nigeria.
Kabla hajachaguliwa kuongoza Nigeria mwaka 2015, Rais Muhammadu Buhari, aliahidi kutokomeza umaskini na kukabiliana na ufisadi.
Lakini, wasiwasi juu ya ufanisi wa mpango huo, ni kwamba hamna tarakimu ya sasa ya idadi nzima ya watu wote wa Nigeria.
Inakisiwa kuwa taifa hilo lenye idadi kubwa zaidi ya watu barani Afrika lina zaidi ya watu milioni 170.
Uchumi wa Nigeria umeporomoka pakubwa baada ya kuanguka kwa bei ya mafuta duniani.
Chanzo cha habari BBC
Post a Comment